Powered By Blogger

Karibu/Welcome

mambo?!

Sunday, January 11, 2009

Nimwambieje?

Nimepokea e-mail ya kwanza, kutoka kwa mwanadada anonymous. Kwa kuwa Blog yetu ni ya faida kwa wote, nimepunguza makali ya baadhi ya maneno. Soma Chini.

Dr Wannabe
Naomba unipe nafasi nina tatizo na bwana wangu ambaye nimeishi naye miaka minne. Tulipoanza uhusiano alikuwa na mwili mzuri, kifua kimejaa misuli na tumbo tambarare. Alikuwa akiishi pekeyake, tumeishi pamoja miaka mitatu na sasa hanivutii tena kimapenzi kwani tumbo limezidi, na hutokwa majasho na kuhema sana tunapokutana, na tumbo linamzuia kunifikia. Napenda mwanaume mwenye kifua cha simba, sasa hivi naweza kumvisha sidiria ndogo. najilaumu kwa kumpikia, je nifanyeje kumwambia bila kumkasirisha?.

Asante Anon, Russia.

RESPONSE:
Hongera kwa kuwa wa kwanza kutuma swali zuri. Usijilaumu kwa kumpenda hapo awali, lakini najiuliza ulimpendea nini?. Kama ulimpendea mwili peke yake?. Najiuliza maswali mengi ambayo ni challenge ya kwanza ya kutoa counseling kwa njia hii...sipati picha kamili. Nitajaribu kadri ya uwezo wangu. Sijui umri wako, uamuzi wako katika mapenzi kama ni mwili tu, labda unapendelea tu company na kustareheshana punde mnapotaka. Hakuna ubaya, lakini kama ni hivyo hakukuwa na haja ya kuishi naye kama mke na mume. Kama unampenda zaidi ya mwili tu na unajali afya yake, na unafikiri kuishi naye daima ama muda mrefu mungu akubariki. Kuna good news! Anaweza kurudi kama awali endapo ataanza kula vizuri na kufanya aina ya mazoezi yatakayofanya mwili uwe katika hali nzuri kiafya. Afanye mazoezi ya resistance, na cardio. Kubeba vyuma au mazoezi yoyote yanayo challenge misuli ya mwili against gravity. Push ups na Chest presses zitajenga kifua cha simba, cardio zitamaliza kule kukuhemea. Je wewe mwenjewe uko katika good shape?. Jinsi ya kumshauri ni kuanza kumpikia chakula cha kiafya, punguza mafuta mafuta, vitamtam. Muombe akusindikize kufanya mazoezi, fanya naye wote mtafaidika. mnunulie kitabu cha mazoezi au vifaa na umsifie anavyopendeza kadri anavyofanya mazoezi. Wote mtafaidika na mtafaidi kufanya mapenzi. By the way, every 35 pounds he loses he will gain 1 inch of penis length. Itakufikia barabara!. Natumai nimesaidia.

PS. Jiulize tena kama uko tayari kuwa naye muda mrefu, na kama kuna zaidi ya mwili wake unachokipenda zaidi. Jiulize ni mwanaume wa aina gani unayemtaka na kumhitaji. He might be the one if you look deep inside you, if not...baby u might want to find another man that you care for deeper than his outer shell. Kwani he's likely to get even fatter sooner or later even if he gets back in shape now.

4 comments:

Mzee wa Changamoto said...

Karibu sana Dr Wanna Be. Karibu katika ulimwengu wa ku-blog. Ulimwengu ambao umetokea kuelimisha, kuburudisha, kufahamisha na kuikomboa jamii. Naona umeanza kwa umakini na naamini utaendelea na darasa la namna hii. Basi karibia kwenye majamvi mengine nako utoe maoni na pia kuchota yale ambayo waweza kuyaeleza kwa namna ama ufasaha zaidi kwa manufaa ya wale wote tusomao blogs.
Narudia tena kuwa KARIBU na KAZI NJEMA

Anonymous said...

Hongera Dr, lakini nadhani ni good idea kama utabadilisha rangi ili web ivutie zaidi. Rangi nyeusi inaumiza macho.....

Other than that i like the contents.
www.jamii1.blogspot.com

Anonymous said...

i say Dr. mimi nauliza hiyo bendera ya nchi gani au labda niko Colour blind)

Anonymous said...

Naona ulikuwa unamtaka kimwili sio kumpenda, maana kumpenda mtu kwa kila kitu na kama hakufikishi lazima ufikiria namna gani ili tufurahishe, kuhusu swala ya umbo apo ndio umepotea maana leo hii ndio miaka miwili je baada ya miaka kumi itakuwaje wakati mwingine usifikia ngono tu. kama ndio ngono basi tafuta ndogo uliomzidi miaka tano au kumi pia ujuwe toy boy wanapenda njee sana kwa hiyo shikilian mtu wako mpe mjo mjema yaani health food na mazoezi kidogo kama kutembea tembea pamoja ili mkirudi home mnakuwa na hamu ya mambo...